Hii ni kwa mujibu wa msomi maarufu wa Kiislamu nchini Iran Hujjatul Islam Mehrdad Koushki, ambaye aliongeza kuwa Itikafu ni zoezi la kiroho na tendo la ibada ambalo lina athari kubwa kwa washiriki.
Ibada hii huongeza mtazamo wa kiroho wa mtu na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu, na huleta hali ya amani ya ndani ya nafsi, alisema.
Aidha, inawasaidia watu kudhibiti msongo wa mawazo na wasiwasi na kwa kuwa Itikaf hufanyika kwa vikundi, inaongeza uwezo wa mtu kufanya kazi katika mazingira yaliyoandaliwa na huimarisha uhusiano wa kijamii, alisema kiongozi huyo wa kidini.
Hujjatul Islam Koushki aliendelea kusema kuwa Itikafu ni fursa ya tafakari na umakini, ikiwasaidia watu katika kuchagua njia yao na kufanya maamuzi ya baadaye.
“Itikafu ina jukumu muhimu katika kutofautisha kati ya mema na mabaya. Zaidi ya hayo, kupitia uhusiano na ukaribu uliojengwa na Muumba, na kuathiriwa na dua zilizotolewa kwa Ahl-ul-Bayt (AS), Itikafu inakuza hisia ya marekebisho, toba, na matumaini ndani ya mtu, ikimuelekeza katika kuboresha na kuwa na matumaini kwa ajili ya siku zijazo.”
Itikafu ni mila ya Mtume Muhammad (SAW) na familia yake yaani Ahul Bayt (AS), na inachukuliwa kama tendo la ibada lenye thawabu kubwa katika Uislamu.
Ni zoezi la kiroho katika Uislamu linalojumuisha kukaa msikitini kwa siku kadhaa, kufunga na kumwomba Mwenyezi Mungu.
Katika mwezi wa Rajab itikafu maalumu hufanyika tarehe 13, 14, na 15. Rajab ni mwezi wa saba wa kalenda ya Kiislamu, na siku za Itikafu mwaka huu zinaangukia tarehe 14, 15, na 16 Januari.
3491409