IQNA

Hafla ya Maadhimisho ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu Jijini Tehran

IQNA – 11 Februari 2026, imesadifiana na maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Wananchi wa Tehran, sawa na mamilioni ya wananchi katika miji mingine kote nchini Iran, wameonesha uaminifu wao kwa misingi na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu kupitia ushiriki wao mkubwa na wa hamasa katika maandamano ya kitaifa ya kuadhimisha tukio hili.

Uwepo huu mpana wa wananchi umeakisi mshikamano wa taifa la Iran, utiifu wao kwa uongozi wa Mapinduzi, na azma yao thabiti ya kulinda maadili ya Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na uhuru na heshima ya nchi yao.

Habari zinazohusiana