IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa

Matembezi ya 22 Bahman yatakuwa ni muhuri wa ushindi wa wananchi wa Iran ya Kiislamu dhidi ya njama za maadui

16:53 - February 10, 2023
Habari ID: 3476541
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema kuwa, matembezi ya Bahman 22 (Febrauri 11) ambayo yatafanyika kesho Jumamosi katika kona zote za Iran kuadhimisha mwaka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu yatakuwa ni muhuri wa ushindi wa wananchi wa Iran ya Kiislamu dhidi ya njama zote za maadu

 Ayatullah Ahmad Khatami ameyasema hayo leo katika khutba za Sala ya Ijumaa ya hapa Tehran na kuongeza kwamba, kuwa na imani na Mwenyezi Mungu huleta ushindi na matumaini katika kila jambo kwani Allah ni Muweza wa kila kitu.

Aidha amesema, baraka nyingine iliyomo kwenye kuwa na imani madhubuti na Mwenyezi Mungu ni kuvunja majivuno na ghururi. Mtu anayetambua uwezo na nguvu za Allah, anapaswa kutozipa nafasi hata chembe ghururi na majivuno. 

Vile vile amesema, kuporomoka utawala wa miaka 57 wa Kipahlavi nchini Iran hakukutokana na jambo jingine isipokuwa nguvu za Mwenyezi Mungu. Ajenda kubwa ya utawala huo wa kitaghuti ilikuwa ni kupiga vita uhuru, dini na imani ya Mwenyezi Mungu huku rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter akiuita utawala huo kwa jina la kisiwa cha amani.

Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, Marekani imevamia nchi 25 duniani kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja, lakini haijathubutu kuishambulia kijeshi Iran katika kipindi cha miaka 43 iliyopita.

Khatibu huyo wa muda wa Sala ya Ijumaa ya Tehran pia amesema, hakuna nchi yoyote iliyoweza kupata ustawi kama wa Iran wa miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika mazingira kama iliyo nayo Jamhuri ya Kiislamu na kwamba ni jukumu la kidini na kitaifa kushiriki katika maadhimisho ya Bahman 22 hiyo kesho kwani huko ni katika kumshukuru Allah kwa neema Zake.

412110

captcha