IQNA

Mwanaharakati wa Nigeria

Mapinduzi ya Kiislamu yaliwakomboa waliokandamizwa na mabeberu

20:31 - February 08, 2023
Habari ID: 3476531
TEHRAN (IQNA) - Mwanaharakati wa Nigeria anasema Mapinduzi ya Kiislamu yakiongozwa na Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu- yaliwakomboa watu waliokuwa wamekandamizwa na madola ya kibeberu ya Magharibi na kambi ya Kikomunisti.

Hayo yamebainika katika Warsha ya kimataifa inatazamiwa kufanyika siku ya Jumatano kwa njia ya intaneti kwa lengo la kujadili Mapinduzi ya Kiislamu. Warsha hiyo imeandaliwa na shirika la habari la IQNA kwa mnasaba wa maadhimisho yam waka wa 44 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Zeenat Ibrahim, mwanaharakati wa Nigeria na mke wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, amesema katika warsha hiyo kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yamekuja katika hali ambayo Waislamu duniani kote walikuwa wamefedheheka kwa sababu ya propaganda za mabeberu.

"Propaganda za wakati ule ziliwafanya Waislamu kuhisi kitu chochote ambacho kinahusishwa na Uislamu kinachukuliwa kuwa ni cha kubakia nyuma na kisichostaarabika." Amesema wakati wa Mapinduzi ya Kiisalmu kulikuwa na kambi mbili za Magharibi na Ukomunisti na wengi  walikuwa wakihisi kwamba hakuna namna Uislamu unaweza kurudi na kutawala.

"Ilikuwa wakati huu ambapo fahari ya Waislamu ilikuwa imekanyagwa na karne nyingi za kutawaliwa na ubeberu na ukoloni. Katika hali hiyo mapinduzi matukufu yalifanikiwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na Imamu. Khomeini alikuwa akimtegemea Mwenyezi Mungu tu. Utegemezi wake kwa Mwenyezi Mungu ulikuwa uti wa mgongo wa harakati yake," alisisitiza.

Hii hapa ni klipu kamili ya hotuba yake.

Wazungumzaji wengine wa hafla hiyo ni mshauri wa rais wa Iran katika masuala ya vyuo vya Kiislamu au Hauza Hujjatul Islam Mohammad Haj-Abolghasemi, naibu waziri wa ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Seyyed Mahdi Farahi, msomi wa Lebanon na mjumbe wa baraza la kisiasa la Hezbollah Bilal Al-Laqis.

3482401

captcha