IQNA

Muujiza wa mahudhurio ya tarehe 11 Februari ulikuwa taswira iliyo wazi ya Iran yenye nguvu

14:49 - February 13, 2026
Habari ID: 3481930
IQNA-Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa maadui, kupitia vitisho vya moja kwa moja vya kijeshi na maonyesho ya nguvu za manowari zao katika eneo, walilenga kuvunja azma ya wananchi wa Iran. Lengo lao lilikuwa kusababisha kupooza kwa uchambuzi wa kisiasa, kuvuruga mizani ya mahesabu ya kijamii miongoni mwa wananchi, na kuchochea hali ya kutoridhika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IQNA, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran wiki hii alikuwa Hujjat al-Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari, katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini (MA).

Hujjat al-Islam Haj Ali Akbari amesema kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, muujiza wa mahudhurio ya wananchi katika tarehe 11 Februari (22 Bahman) umeangusha mipango yote ya maadui.

Ameongeza kuwa, ushiriki wa makumi ya mamilioni ya watu kote nchini siku ya Jumatano,, ikiwemo angalau watu milioni mbili na nusu jijini Tehran, ulitoa taswira iliyo wazi ya Iran yenye nguvu na uthabiti, na ukaionesha dunia nzima maana ya kweli ya nguvu ya kuzuia (deterrence) inayotokana na mshikamano wa kitaifa na uwepo wa umma katika maisha ya taifa.

Akiashiria vita vya kichokozi vya siku 12 vya Israel na Marekani dhidi ya Iran mwezi Juni mwaka jana, Hujjat al-Islam Haj Ali Akbari amesema kuwa, baada ya vita hivyo na kufuatia machafuko ya hivi karibuni, maadui walianzisha “operesheni nzito” dhidi ya wananchi wa Iran katika fremu ya vita vya kisaikolojia na propaganda.

Amesema operesheni hiyo ilihusisha, miongoni mwa mambo mengine, takwimu za uongo, madai ya kupotosha, simulizi zisizo za kweli kwa kutumia watu maarufu wakiwemo  wasanii na wanamichezo pamoja na shinikizo kwa wafanyabiashara na makundi ya kijamii. Ameongeza kuwa kulikuwa pia na shinikizo la kimataifa, vikwazo vinavyojirudia, na maonesho ya kisiasa ya nchi za Ulaya ambazo ni vibaraka.

Khatibu huyo wa Ijumaa amesisitiza kuwa nchi hizo za Ulaya, hasa Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani, zimeshiriki katika uhasama dhidi ya Iran, iwe ni katika vita vya siku 12 au “fitna ya Kizayuni” ya hivi karibuni ambayo wachochezi wake wakuu walikuwa pia ni Marekani na Israel.

Habari inayohusiana:

Katika sehemu nyingine ya khutba zake, Hujjat al-Islam Haj Ali Akbari amewakumbusha waumini kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unakaribia. Kwa msingi huo amewataka Waislamu kujiandaa kwa mwezi huo mtukufu, aliouelezea kuwa ni mwezi bora zaidi katika miezi ya Mwenyezi Mungu, ambamo waumini wanaalikwa kwenye dhifa ya Mola wao.

Amesisitiza umuhimu wa kuwa na mpango wa kiroho kabla ya kuingia Ramadhani, akihimiza maandalizi yanayozingatia maelekezo ya Ahlul Bayt (AS), ili kuuingia mwezi huo kwa maisha yenye kujisitiri, utakaso wa akili na fikra, usafishaji wa nyoyo, na kuimarisha uhusiano wa kiroho baina ya mja na Mwenyezi Mungu.

4334200

captcha