IQNA

Mapinduzi ya Kiislamu

Mamilioni ya wananchi wa Iran washiriki maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

19:05 - February 11, 2024
Habari ID: 3478334
IQNA-Mamilioni ya wananchi wa Iran wameshiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 kwa uongozi wa Imamu Ruhullah Khomeini (MA).

Maandamano hayo yaliyoambatana na sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamefanyika leo katika miji mbalimbali ya Iran.

Katika mji mkuu Tehran washiriki wameonekana wakiwa wamebeba mabango na maberamu ya kuilaani Marekani, utawala haramu wa Israel na washirika wao na jumbe nyingine zinazosisitiza kusimama kidete taiifa hili dhidi ya maadui wa mapinduzi haya.

Matembezi au maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran yameisia katika Mzunguko wa Azadi ambapo Rais Ebrahim Rais amelihutubia taifa.

Ikumbukwe kuwa, miaka 45 iliyopita katika siku kama ya leo 22 Bahman Hijria Shamsia sawa an 11 Februari, Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote.

Siku hiyo wananchi waliokuwa wakipiga takbira na kutoa nara za kimapinduzi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung’oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. Hatimaye utawala wa kifalme uliotawala Iran kwa miaka 2500, uliangushwa na mfumo wa Kiislamu unaotegemea kura ya wananchi ukaanza kutawala Iran Februari mwaka 1979.

3487151

Habari zinazohusiana
captcha