IQNA

Mapinduzi ya Kiislamu

Kiongozi Muadhamu: Maadhimisho ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yamedhihirisha umoja wa Wairani

11:52 - February 13, 2025
Habari ID: 3480206
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Iran kwa kufikisha "ujumbe wa umoja" kwa jamii ya kimataifa katika maadhimisho ya miaka 46 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kihistoria ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.

Ayatullah Ali Khamenei ametoa pongezi hizo Jumatano hapa mjini Tehran alipohutubia hadhara ya maafisa wa Wizara ya Ulinzi, wasomi wa sekta ya ulinzi, wataalamu na wafanyakazi wa wizara hiyo, pamoja na familia za Mashahidi wanaotoka katika sekta hiyo ya ulinzi ya nchi hii.

Kiongozi Muadhamu ameitaja siku ya kuadhimisha Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa moja ya matukio muhimu zaidi ya kitaifa, yanayoonyesha umoja na nguvu ya wananchi wa Iran licha ya mashinikizo kutoka nje.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, sherehe za maadhimisho ya mwaka huu hazikuwa tu kumbukumbu, bali ni kitendo chenye nguvu cha Muqawama na umoja wa kitaifa.

Amebainisha kuwa, "Huu ulikuwa ujumbe wa umoja kutoka kwa watu wa Iran. Licha ya vitisho vya mara kwa mara na vya kipuuzi dhidi yetu, wananchi wa Iran wameonyesha ulimwengu utambulisho wao, nguvu zao na azimio lao lisiloyumba."

“Hakika watu waliamka siku ya Jumatatu wakaingia mitaani na mabarabarani, wakitoa nara, huku wakitoa maoni yao kwenye vyombo vya habari, na hii ilitokea nchi nzima. Ilikuwa hamasa ya wananchi, na harakati kubwa ya kitaifa,” amesema Imam Khamenei.

Ameeleza bayana kuwa: "Siku zote nasisitiza kwa hadhira yangu, kwa vijana wapendwa ambao nimefungamana nao sana na kujitolea kwao, kwamba hatua lazima zichukuliwe kwa wakati unaofaa. Taifa la Iran lilichukua hatua kwa wakati mwafaka siku ya Jumatatu; wamefanya yale ambayo yalihitaji kufanywa hasa, na kwa wakati yalihitajika kufanywa. Wamejitokeza kwa wakati ufaao.”

KadhalikaJumatano, Kiongozi Muadhamu ametembelea Maonyesho ya Kijeshi ya  Eqtedar (Nguvu) 1403, ambayo yalionyesha mafanikio na uwezo wa hivi karibuni wa sekta ya ulinzi ya Iran. Maonyesho hayo yameonyesha zana na vifaa vya hali ya juu na teknolojia mpya zinazotumiwa katika maeneo kama vile ulinzi wa anga, makombora ya balestiki na ya cruise, zana erevu, anga za mbali, ndege zisizo na rubani, mawasiliano na nishati.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza bayana kwamba, marafiki wa Iran wanajivunia uwezo wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu, katika hali ambayo maadui wa taifa hili wanaogopa na kutiwa kiwewe na uwezo huo.

Ayatullah Khamenei amesema, “Suala la kulinda taifa, kulinda usalama si jambo dogo. Leo, nguvu ya ulinzi ya Iran inatambulika na inajulikana sana. Marafiki wa Iran wanajivunia nguvu hii ya ulinzi, na maadui wa Iran wanaiogopa. Hili ni muhimu sana kwa taifa, na kwa nchi.”

3491845

Habari zinazohusiana
captcha