mapinduzi ya kiislamu

IQNA

IQNA-Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesisitiza kuwa maadui, kupitia vitisho vya moja kwa moja vya kijeshi na maonyesho ya nguvu za manowari zao katika eneo, walilenga kuvunja azma ya wananchi wa Iran. Lengo lao lilikuwa kusababisha kupooza kwa uchambuzi wa kisiasa, kuvuruga mizani ya mahesabu ya kijamii miongoni mwa wananchi, na kuchochea hali ya kutoridhika.
Habari ID: 3481930    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/13

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewasifu na kuwapongeza wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi kote nchini katika maandamano ya maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa maandamano hayo yamewakatisha tamaa maadui.
Habari ID: 3481929    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/13

IQNA – 11 Februari 2026, imesadifiana na maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Wananchi wa Tehran, sawa na mamilioni ya wananchi katika miji mingine kote nchini Iran, wameonesha uaminifu wao kwa misingi na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu kupitia ushiriki wao mkubwa na wa hamasa katika maandamano ya kitaifa ya kuadhimisha tukio hili.
Habari ID: 3481927    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12

IQNA – Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamegeuka kuwa mfano hai wa kuunganisha dini, maisha ya kijamii na maendeleo katika ulimwengu wa kisasa, amesema mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa kutoka Lebanon.
Habari ID: 3481925    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/12

Rais Pezeshkian katika hotuba ya maandamano ya tarehe 22 Bahman:
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika maadhimisho ya Siku ya Allah ya tarehe 22 Bahman (Februari 11), amesema kuwa Iran haitaki kumiliki silaha za nyuklia, jambo ambalo imelitangaza wazi, na iko tayari kwa aina zote za uhakiki wa kimataifa. Ameongeza kuwa ukuta mkubwa wa kutokuaminiana uliowekwa na Marekani umezuia mazungumzo kufikia matokeo yenye maana.
Habari ID: 3481920    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/11

Mamilioni ya wananchi kutoka matabaka yote ya kijamii wamejitokeza mitaani kote nchini Iran kushiriki maandamano ya kitaifa yanayoashiria maadhimisho ya miaka 47 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3481919    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/11

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa wito kwa taifa la Iran kuonyesha irada, azma thabiti na kusimama kidete, kwa kushiriki kwa wingi katika matembezi na mijumuiko ya kuadhimisha miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu, akisema kuwa umoja huo utamkatisha tamaa adui wa nchi hii.
Habari ID: 3481912    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/10

IQNA – Profesa mmoja wa Chuo Kikuu kutoka Iraq ameyalezea Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran si tu kama tukio la kisiasa, bali kama mabadiliko makubwa katika mantiki ya madaraka na ufahamu wa Ummah ya Kiislamu.
Habari ID: 3481894    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/07

IQNA-Jumuiya ya Wasomi wa Kiislamu wa Yemen imetangaza mshikamano wake kamili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kutaka ulimwengu wa Kiislamu kuchukua msimamo wa pamoja katika suala hilo.
Habari ID: 3481879    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/02/01

IQNA – Mamilioni ya wananchi nchini Iran waliandamana Jumatatu kulaani ghasia za hivi karibuni zilizochochewa na makundi ya kigaidi yanayodaiwa kuungwa mkono na Marekani na utawala wa Kizayuni.
Habari ID: 3481796    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amepongeza maandamano ya kitaifa yaliyoonyesha uungaji mkono kwa Jamhuri ya Kiislamu, akisema wingi wa wananchi waliojitokeza “umeandika historia” na kuvuruga njama za maadui waliolenga kuibua misukosuko kupitia vibaraka wao wa ndani.
Habari ID: 3481795    Tarehe ya kuchapishwa : 2026/01/13

IQNA – Mwanazuoni mwandamizi kutoka Iran amesema kuwa kulinganisha mtazamo wa Tauhidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na mtazamo wa kisekula wa Magharibi kunasaidia kufichua kwa undani vipengele vya migogoro ya dunia ya leo.
Habari ID: 3481185    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/05

IQNA – Mamilioni ya Wairani walijitokeza mitaani kote nchini Februari 10, 2025, kuadhimisha miaka 46 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3480207    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/13

Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Iran kwa kufikisha "ujumbe wa umoja" kwa jamii ya kimataifa katika maadhimisho ya miaka 46 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kihistoria ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979.
Habari ID: 3480206    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/13

IQNA – Semina ya kitamaduni na kielimu iliyopewa jina “Utangulizi wa Mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu katika Nyanja ya Wanawake” iliandaliwa jijini Dar es Salaam, Tanzania, Jumatatu.
Habari ID: 3480205    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/02/12

Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi amesema: Jamhuri ya Kiislamu inaongoza mapambano dhidi ya ugaidi na kutetea haki za binadamu.
Habari ID: 3478335    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/11

Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Mamilioni ya wananchi wa Iran wameshiriki katika maandamano ya kuadhimisha miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyotokea mwaka 1979 kwa uongozi wa Imamu Ruhullah Khomeini (MA).
Habari ID: 3478334    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/11

Mtazamo
IQNA - Imam Khomeini (MA) alitilia mkazo hadhi ya juu ya wanawake katika Uislamu na alizingatia sana haki zao, mwanazuoni wa Algeria amesema.
Habari ID: 3478322    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/02/09

Mapinduzi ya Kiislamu
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kadhia kuu nambari moja ya Ulimwengu wa Kiislamu ni Palestina na ukombozi wa Quds Tukufu, Kibla cha Kwanza cha Waislamu, kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3478281    Tarehe ya kuchapishwa : 2024/01/31

TEHRAN (IQNA) – Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky alikaribishwa kwa furaha na umati mkubwa wa watu mjini Tehran.
Habari ID: 3477718    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/12