IQNA

Sheikh Ali Salman:

Kamatakamata ya kisiasa haitatatua mgogoro wa Bahrain

17:15 - July 28, 2012
Habari ID: 2378940
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kitaifa ya Bahrain al-Wifaq amesisitiza katika hotuba kwamba kamatakamata ya kisiasa inayoendeshwa na utawala wa nchi hiyo haitatatua mgogoro wa nchi hiyo bali itaondoa kabisa uwezekano wa kutatuliwa kwake kwa njia za kisiasa.
Sheikh Ali Salman amesema kwamba kuna nchi kadhaa za eneo la Mashariki ya Kati ambazo zimetangaza kuwa tayari kupatanisha pande zinazohasimiana nchini Bahrain lakini watawala wa ukoo wa Aali Khalifa wamekataa na kupinga suala hilo. Amesema kamwe wananchi wa Bahrain hawataacha kufuatilia na kupigania matakwa yao halali kutoka kwa watawala wa nchi hiyo na kwamba hatua ya utawala wa Manama ya kupinga maandamano halali ya wananchi katika mji huo ni jambo lisilokubalika kimantiki wala kisheria.
Sheikh Salman amesema maslahi ya kiuchumi yanayotumiwa na watawala hao kama kisingizio cha kupinga maandamano, hayako juu ya matakwa ya wananchi.
Katibu Mkuu huyo wa al-Wifaq akiashiria suala hili kwamba mazungumzo ndiyo njia pekee ya kutatuliwa matatizo ya Bahrain ameongeza kuwa wananchi wa Bahrain wataunga mkono mazungumzo hayo iwapo tu yatadhamini na kuheshimu matakwa ya wananchi la sivyo hayatakuwa na maana. 1063353
captcha