IQNA

“Siku 500 za Dhulma”: Amnesty International yalaani Israel kwa kuendelea kumzuilia daktari wa Kipalestina

15:08 - May 12, 2026
Habari ID: 3482229
IQNA – Katika kumbukumbu ya tukio lenye kuhuzunisha, shirika la Amnesty International limeilaani vikali utawala wa Israel kwa kuendelea kumshikilia daktari wa Gaza, Dkt. Hussam Abu Safiya.

Afisa mwandamizi wa Amnesty International ameishutumu Israel kwa kuendelea kumweka kizuizini Dkt. Abu Safiya, akisema ni “siku 500 za kizuizi cha kiholela” na “siku 500 za dhulma.”

Erika Guevara Rosas, Mkurugenzi Mwandamizi wa Utafiti, Utetezi, Sera na Kampeni wa Amnesty International, aliandika kwenye mtandao wa X siku ya Jumatatu akieleza masaibu ya wahudumu wa afya wa Kipalestina wanaoendelea kuadhibiwa kwa sababu tu ya kuokoa maisha chini ya mashambulizi makali ya mabomu ya Israel.

“Wahudumu wa afya wanaadhibiwa kwa kuokoa maisha,” Rosas aliandika, huku akiitaka serikali ya Tel Aviv “imwachilie mara moja na bila masharti yoyote” Dkt. Abu Safiya pamoja na wataalamu wote wa afya wa Kipalestina waliowekwa kizuizini kiholela.

Hata baada ya shambulio la angani la Israel kumuua mwanawe, daktari huyo mwenye kujitolea hakuwahi kuwageuka wagonjwa wake, akidhihirisha uthabiti na moyo usiovunjika wa wahudumu wa afya wa Gaza mbele ya ukatili unaowakumba.

Ripoti za kuaminika zilizopokelewa na Waandishi Maalumu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Tlaleng Mofokeng na Prof. Ben Saul, mwezi Machi, zilibainisha kuwa Dkt. Abu Safiya ameteswa na kunyimwa huduma za afya kimakusudi, hali inayoweka uhai wake katika hatari kubwa.

Hata hivyo, Marekani na washirika wake wa Magharibi wamesalia kimya bila kuchukua hatua yoyote ya kuzuia yale yanayoendelea kufanywa na utawala wa Tel Aviv.

Shirika moja la haki za binadamu lenye makao Uingereza liliielezea tukio hilo la kutekwa kama sehemu ya sera ya makusudi ya Israel ya kuwanyanyasa na kuwadhuru wahudumu wa afya wa Kipalestina, sambamba na kuvuruga mfumo mzima wa huduma za afya Gaza—hatua ambazo, kwa mujibu wa wachambuzi, zinaonekana kuunda mazingira ya kuangamiza uwezo wa watu wa Palestina kuendelea kuishi.

Tangu utawala wa Kizayuni uzindue vita vyake dhidi ya Gaza mwezi Oktoba 2023, angalau wahudumu wa afya 737 wa Kipalestina wamekamatwa kiholela. Katika kipindi hicho hicho, zaidi ya 1,722 wameuawa, wastani wa zaidi ya wawili kwa siku.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limerekodi zaidi ya mashambulio 930 dhidi ya miundombinu ya afya ya Gaza, yakiacha hospitali zote 36 zikiwa zimeharibiwa au kutokuwepo tena kabisa, huku nusu tu zikisalia kufanya kazi kwa kiwango kidogo mno.

Ukosefu wa usalama huu na mashambulizi haya ya kikatili vinaonekana kuwa sehemu muhimu ya kampeni pana inayoelekezwa kuvunja kabisa mfumo wa huduma za afya wa Gaza, na hivyo kudhoofisha uwezo wa watu wa Palestina kuendelea kuhimili maisha.

3497428

Habari zinazohusiana
captcha