
Kwa sasa, zaidi ya mahujaji wa Iran 22,000 wako mjini Makka, na waliobakia miongoni mwa mahujaji wa nchi hiyo wako Madina.
Kwa kuanza kwa mwezi mtukufu wa Dhul-Hijjah, mji wa Madina utakuwa hauna tena mahujaji wa Iran ifikapo mwishoni mwa juma hili, huku mahujaji walioko Makka wakijiandaa kutekeleza ibada ya Hija.
Baada ya kutekeleza manasiki ya Hija, na kwa kuzingatia kwamba mahujaji wote wa Iran walifika kwanza Madina, wataanza kurejea nchini kwa awamu kadhaa kuanzia tarehe 1 Juni.
Hija ni safari ya ibada kwenda Makka ambayo kila Muislamu mwenye uwezo wa kimwili na wa kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.
Ibada hiyo ya kila mwaka inahesabiwa kuwa ni miongoni mwa nguzo za Uislamu na ndiyo mkusanyiko mkubwa zaidi wa hija ya pamoja duniani.
Vilevile, Hija ni dhihirisho la umoja wa Waislamu na unyenyekevu wao mbele ya Allah (SW).
3497522