
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA , Chuo hicho cha kimataifa cha masomo ya Kiislamu kilichoko Qom nchini Iran, ambacho hupokea wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali, kilitoa kauli hiyo kujibu msimamo wa kupinga Iran uliotolewa na Chuo Kikuu cha Al-Azhar cha Misri,
Katika vita vya uchokozi visivyochokozwa vilivyoanzishwa tarehe 28 Februari na muungano wa kijeshi wa Marekani na Israel, Iran ilijibu kwa kujilinda kupitia mashambulizi mengi ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya maslahi ya Marekani na Israel katika eneo hilo, hasa katika mataifa ya Ghuba ya Uajemi ikiwemo UAE.
Hata hivyo, Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilionekana kuikosoa Tehran na kulaani kile kilichokiita “mashambulizi yasiyo na uhalali” ya Iran dhidi ya UAE na mataifa mengine ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi. Al Azhar pia iliitaka Iran kusitisha mara moja mashambulizi yake ya kulipiza kisasi dhidi ya ngome za kijeshi na kiuchumi za Marekani katika nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.
Katika kujibu msimamo huo wa Al Azhar, a Chuo Kikuu cha Al-Mustafa kimeendelea kubaini kuwa: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kuanzisha vita vyovyote, na hatua zake za kijeshi za hivi karibuni zimekuwa ni majibu halali ya kujihami na kuzuia madhara kufuatia mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya usalama na mamlaka ya ardhi ya Iran kupitia matumizi mabaya ya maeneo ya baadhi ya nchi jirani, ikiwemo UAE.”
Chuo hicho pia kimesisitiza kuwa Iran imeendelea kushikamana na misingi ya busara, diplomasia na ujirani mwema, huku kikitoa wito kwa Al-Azhar kutathmini matukio kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na Sunnah badala ya kuathiriwa na “mazingira ya propaganda za vyombo vya habari na wanasiasa wanaoegemea Magharibi.”
Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Chuo Kikuu cha Al-Mustafa kimesisitiza umuhimu wa maadili ya Kiislamu wakati wa vita.
Taarifa hiyo imesema: “Kwenye operesheni zake za kujibu mashambulizi, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran , tofauti na mwenendo wa kihalifu wa utawala wa Israel na wanaounga mkono , haikulenga raia wasio na hatia wala miundombinu muhimu ya kiraia ya nchi mbalimbali, na malengo halali ya operesheni hizo yalikuwa kambi za kijeshi za Marekani katika eneo hilo,”
“Pale ambapo adui alitumia miundombinu ya nchi zilizotajwa kuharibu miundombinu ya Iran, hatua za kulipiza zilichukuliwa kwa mujibu wa kanuni ya Qur’ani ya kulipiza kisasi."
Chuo hicho kimetoa wito kwa mataifa yote ya Kiislamu kuungana dhidi ya maadui wawili ambao ni Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, huku kikiwahimiza wasomi na viongozi wa fikra katika ulimwengu wa Kiislamu kuzuia njama za mgawanyiko zinazopangwa na tawala hasimu.
Aidha, kiliwataka watawala wa nchi ambazo zimeruhusu maeneo yao kutumiwa na “makafiri” kufanya mashambulizi dhidi ya taifa jingine la Kiislamu kukomesha “dhambi hiyo kubwa.”
UAE iliruhusu ardhi yake na miundombinu yake ya vifaa kutumiwa, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kusaidia operesheni za kijeshi na kijasusi za Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Chuo Kikuu cha Al-Mustafa kilisema kimesema: “Ushiriki, uwezeshaji na kuandamana kwa Umoja Falme za Kiarabu katika uchochezi wa vita wa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran kunabeba hukumu ya kifiqhi ya ‘uasi’ (ṭughyān), na kusaidia kambi ya ukafiri dhidi ya ndugu Waislamu ni haramu kabisa,”
Katika ripoti iliyochapishwa Jumanne, gazeti la Wall Street Journal likinukuu vyanzo vyenye taarifa, lilisema kuwa UAE ilifanya mashambulizi yake ya kijeshi dhidi ya Iran kwa kuunga mkono moja kwa moja vita vya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, moja ya mashambulizi hayo yalilenga kiwanda cha kusafisha mafuta katika kisiwa cha Lavan kwenye Ghuba ya Uajemi mwezi Aprili, karibu na kipindi ambacho makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili yaliyosimamiwa na Pakistan yalifikiwa kati ya Washington na Tehran.
Katika kipindi cha vita hivyo, UAE na Saudi Arabia zote zilifungua vituo vyao vya anga kwa ndege za kivita za Marekani ili kushambulia Iran.
Wakati Rais wa Marekani Donald Trump akidaiwa kufikiria kwa uzito kuanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ameonya hivi karibuni kwamba “Marekani inapaswa kuwa makini isivutwe tena kwenye dimbwi la mgogoro na watu wenye nia mbaya. Hali hiyo pia inaihusu UAE.”
3497446