
Katika ujumbe huo, alimwelezea marehemu Rais Raeisi kama kiongozi aliyekuwa na hisia ya juu ya uwajibikaji, mwenye kuzingatia uadilifu, mwenye kuendesha diplomasia hai na yenye manufaa, na hasa aliyekuwa karibu na wananchi kwa unyenyekevu na huruma.
Ujumbe uliotolewa na ofisi ya Kiongozi Muadhamu siku ya Jumatano uliwaenzi mashahidi wa ajali ya helikopta ya Mei 19. Kiongozi Muadhamu amesema kuwa mashahidi hao ni “ukumbusho wa shahada ya kundi kubwa la watumishi waliotoa maisha yao kwa ajili ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,” akisisitiza kuwa idadi kubwa ya watumishi wa Jamhuri ya Kiislamu wameuawa shahidi..
Katika kutaja mifano ya waliotangulia mbele ya haki baada ya kuuawa shahidi, amewataja wafuatao. Mwanafalsafa mashuhuri Morteza Motahhari aliyeuawa mwaka 1979; Mohammad Hosseini Beheshti, mkuu wa kwanza wa Idara ya Mahakama aliyeuawa mwaka 1981; Mohammad‑Ali Raja’i, rais wa pili aliyeuawa mwaka huo huo; na Mohammad‑Javad Bahonar, waziri mkuu wa pili aliyeuawa mwaka 1981. Pia alimtaja Mohammad Ali Al‑e Hashem, mwakilishi wa Kiongozi katika Mkoa wa Azarbaijan ya Mashariki, pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir‑Abdollahian, waliokufa shahidi wakiwa pamoja na Raeisi katika ajali ya helikopta mwaka 2024. Aidha, alimtaja Ali Larijani ambaye aliuawa katika shambulio la Marekani na Israel tarehe 17 Machi.
Kiongozi Muadhamu amesema alisema: “Kuanzia Motahhari, Beheshti, Raja’i na Bahonar, hadi Raeisi, Al‑e Hashem, Amir‑Abdollahian na Larijani — mamia ya watu mashuhuri walioinukia katika shule ya Imam Khomeini Mkuu na Khamenei mpendwa (Mwenyezi Mungu awapandishe daraja zao), wameupamba wasifu wa utumishi wa dhati na wa Kijihadi i wa maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu kwa saini zao za damu.” Kauli hiyo ilisisitiza mwendelezo wa kizazi hadi kizazi katika kujitolea kwa ajili ya dola ya Kiislamu.
Akizungumzia sifa za Shahidi Rais Raeisi, Ayatullah Mojtaba Khamenei alitaja uwajibikaji wake, mtazamo wake wa kuwawezesha vijana, kujali kwake haki na uadilifu wa kijamii, diplomasia yake iliyokuwa hai na yenye tija, pamoja na ukaribu wake wa dhati na wananchi. Alibainisha kuwa sifa hizi ziliwatia moyo marafiki wa Iran, wakiwemo mujahidina wa mhimili wa Muqawama, na pia wale wote wanaolihurumia taifa. Amesema sifa hizo zilichanganyika na kina cha kiroho kilichotokana na imani thabiti ya Rais Raeisi.
Kiongozi Muadhamu alieleza kuwa uhusiano mwema kati ya viongozi na wananchi huzaa shukrani na kuaminiana kwa pande zote. Aliongeza kuwa ingawa muhula wa Rais Raeisi haukukamilika, kipindi chake kilidhihirisha jitihada, huruma kwa taifa, na dhamira ya kulinda uhuru na heshima ya nchi katika medani ya kimataifa.
Katika sehemu ya ujumbe wake iliyotafsiriwa kulenga Marekani na Israel, Kiongozi Muadhamu alisema: “Leo tunasimama mbele ya matukio ya kishujaa ya taifa la Iran katika muqawama na mapambano yake ya kipekee ya kihistoria dhidi ya majeshi mawili ya kigaidi ya kimataifa."
Amesema hali hiyo inaongeza uzito wa wajibu kwa maafisa wote wa Jamhuri ya Kiislamu , kuanzia uongozi wa juu na wakuu wa mihimili ya dola hadi ngazi zote za usimamiz, ili kulinda maslahi ya taifa na kuendeleza njia ya kujitegemea.
4353369