IQNA

Mijadala ya Imam Ridha (AS)  (AS) /1

Mijadala ya Imam Ridha (AS) na Wafuasi wa Imani na Madhehebu Tofauti

20:14 - September 03, 2024
Habari ID: 3479378
IQNA – Imam Ridha (AS) alifanya midahalo na wanazuoni na watu mashuhuri wa madhehebu za Kiislamu pamoja na dini nyinginezo kwenye mada tofauti na alikuwa mshindi katika midahalo yote.

Abu al-Hassan Ali bin Musa bin Jafar, anayejulikana kama Imam Ridha (AS) na Alim wa Ahul Bayt wa Mtume Muhammad (SAW) ni Imam wa nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia aliyezaliwa mwaka 148 Hijiria (765 Miladia) huko Madina na aliuawa shahidi kwa amriya Khalifa Maamun wa silsila ya watawala wa Bani Abbas  mwaka 203 Hijria (818 AD).

Imam Ridha (AS) alikuwa maarufu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu, uchamungu, unyenyekevu, ukarimu, na ushujaa.

Mijadala ya Fiqhi (sheria za Kiislamu) ilikuwa imeenea kabla ya Imam Ridha (AS) lakini katika zama zake, mijadala ya kiitikadi ilishika kasi zaidi. Vikao vingi vya mijadala vilifanyika ambapo Imam Ridha (AS) alizungumza na wanazuoni wa madhehebu ya Kiislamu na dini nyinginezo kuhusu masuala tofauti.

Kwa madhumuni ya kisiasa, Ma’mun alitaka kuona Imam Ridha (AS) akishindwa katika angalau moja ya mijadala, lakini hakuona hivyo kwa sababu Imam Ridha (AS) alikuwa ndiye mshindi katika vikao vyote vya masomo yote.

Mijadala hiyo ilifichua undani wa ujuzi wa Imam Ridha (AS) kuhusu Uislamu na imani nyinginezo na utetezi wake wa ukweli wa Uislamu. Alitetea ukweli wa Uislamu na akajibu maswali na mashaka, kwa kutumia hoja za busara na Hadithi.

Kwa kueleza mafundisho ya kweli ya Uislamu, alionyesha sura halisi ya dini kwa walimwengu na kuzuia mitazamo isiyo sahihi na yenye misimamo mikali isienee.

Masuala makuu yaliyojadiliwa katika mijadala hiyo ni pamoja na Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), Utume wa Mitume wa Mwenyezi Mungu, hasa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu Muhammad Al Mustafa (SAW), miujiza ya Mitume, hadhi ya Ahl-ul-Bayt (AS) katika Uislamu, na tafsiri ya Qur'ani. .

Kwa kufasiri Qur'an, Imam Ridha  (AS) alijibu maswali na mashaka mengi na akaeleza maana kamili ya aya hizo.

Miongoni mwa mijadala maarufu ya Imam Ridha  (AS) ni ule aliokuwa nao na mwanazuoni mashuhuri wa Kikristo aliyejulikana kama Jathliq, ambaye alishindwa kujibu maswali yaliyoulizwa na Imam Ridha   (AS). Mwingine alikuwa Raas al-Jalut, kiongozi wa Kiyahudi, ambaye alikiri ukweli wa Uislamu na utume wa Mtume wa mwisho wa Mwenyezi Mungu Muhammad (SAW) wakati wa mjadala wake na Imam Ridha  (AS).  

Pia, Herbez, mwanazuoni wa Kizoroastria, alikiri udhaifu katika imani ya Kizoroasta wakati wa mjadala wake na Imam Ridha  (AS).

Mijadala ya Imam Ridha  (AS) ilikuwa na matokeo muhimu kwani ilipelekea kuenea kwa Uislamu na kuwavutia wengi kwenye dini hiyo. Pia waliutambulisha Uislamu halisi duniani na kuzuia kuenea kwa ufahamu wa uwongo na wa itikadi kali wa dini hiyo. Mijadala hiyo pia iliimarisha hadhi ya Ahl-ul-Bayt (AS) katika jamii ya Kiislamu, na kuwasaidia watu wengi kujifunza kuhusu hadhi na maarifa yao tukufu.

3489754

Kishikizo: imam ridha as
captcha