IQNA

Idadi Kubwa ya Wafanyaziyara wafika Karbala katika Siku za Mwisho za Safar

8:11 - August 23, 2025
Habari ID: 3481123
IQNA – Mji mtukufu wa Karbala, Iraq, umefurika wafanyaziyara kwa wingi mno katika siku za mwisho ya mwezi wa Safar, kwenye makaburi matukufu ya Imam Hussein (AS) pamoja na ndugu yake, Hadhrat Abbas (AS).

Kila mwaka katika mwezi wa Safar, Karbala hupokea mamilioni ya wafanyaziyara kutoka ndani na nje ya Iraq, wanaofika kutembelea maqbara mawili matukufu.

Siku za mwisho za Safar huambatana na kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume Mtukufu (SAW), pamoja na kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hassan (AS) na shahada ya Imam Ridha (AS).

Kila tukio kati ya haya, linaleta huzuni kuu na huvutia wafanyaziyara kwa wingi Karbala. Na pale siku hizi zinapokutana na Ijumaa, idadi ya wageni huongezeka zaidi kwa baraka zake.

Miongoni mwa matendo yanayopendekezwa katika Ijumaa ya mwisho ya Safar ni kusoma salawat kwa wingi, kutoa sadaka, kutamka “Allahu Akbar” na “La ilaha illa Allah”. Pia, kuswali rakaa mbili ambapo baada ya Suratul-Fatiha inasomwa Suratul-An’am, ni ibada yenye ujira mkubwa. Kufunga katika siku hizi za mwisho wa Safar pia ni jambo lenye fadhila kubwa.

Hapa chini kuna picha za wafanyaziyara waliokusanyika katika maqbara ya Imam Hussein (AS) na Hazrat Abbas (AS) katika Alhamisi ya mwisho ya mwezi wa Safar:

 

 

4301133

captcha