IQNA

Harakati za Qur'ani

Haram ya Imam Ridha (AS) imeandaa vipindi maalum vya Qur'ani huku mamilioni wakiwasili Mashhad

17:57 - September 03, 2024
Habari ID: 3479375
IQNA - Programu zenye ubunifu za Qur'ani Tukufu zinafanyika katika Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) huku mamilioni ya mahujaji wakiwasili Mashhad kuandaa maandamano ya maombolezo.

Mkurugenzi wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS), ambayo ni maarufu kama Astan Quds Razavi, alielezea shughuli za Qur'ani katika siku kumi za mwisho za mwezi wa Safar zinazojumuisha matembezi na mijumuiko ya maombolezo ya kukumbuka  kuuawa shahidi Imam Ridha (AS).

Hujjatul Islam Seyyed Masoud Mirian alisema kuwa maonyesho katika sehemu moja ya haram hiyo tukufu yanaonesha mafanikio ya  Astan Quds Razavi  katika masuala ya Qur'ani, huku pia yakitoa programu kadhaa za Qur'ani.

Mipango ni pamoja na kufundisha kusoma na kuhifadhi, kufasiri  Qur'ani Tukufu, na pia kujielimisha kuhusu visa vya Qur'ani, kufundisha usomaji kwa sauti, na kukariri aya zilizochaguliwa za Qur'ani.

Mirian ameashiria utekelezaji wa programu maalum za Qur'ani kwa watoto na vijana katika maonyesho hayo. Mwaka huu, kibanda cha burudani cha Qur'ani Tukufu  kina teknolojia ya kidijitali, ikiwa ni pamoja na michezo ya Iran yenye mada kuhusu mashahidi wa Karbala na Gaza, pamoja na michezo ya Qur'ani ya watoto inayotegemea mfumo wa uendeshaji wa Android.

Lengo la programu na michezo hii ni kuwafahamisha zaidi vijana matukio ya Karbala na mafunzo yake, alisema.

Maonyesho hayo yalifunguliwa mnamo Agosti 31, 2024, na yataendelea kwa wiki moja, kutoka nne asubuhi hadi saa 11 jioni.

Maonyesho hayo yanajiri huku mamilioni ya wafanyaziara kutoka mikoa tofauti ya Iran na maeneo mengine duniani wakielekea Mashhad kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ridha (AS), Imam wa nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

3489752

captcha