IQNA

Ahul Bayt (AS)

Qiraa ya Surah Al-Insan katika mkesha wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Imam Ridha (AS)

21:40 - May 18, 2024
Habari ID: 3478842
IQNA - Programu za Qur'ani zitaandaliwa katika mkesha wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ridha (AS) siku ya Jumapili.

Hafla hiyo itafanyika Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS), Imam wa 8 wa Waislamu wa madhehebu ya huko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran na halikadhalika katika maeneo mengine matakatifu na misikiti kote Iran. Hayo ni kwa mujibu wa wa mkurugenzi wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Idara ya  Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) ambayo ni maarufu kama Astan Quds Razavi.

Programu hiyo inajumuisha usomaji wa pamoja wa Surah Al-Insan, sura ya 76 ya Qur’ani Tukufu, Hujjatul-Islam Seyed Masoud Mirian alisema.

Ameongeza kuwa, Astan Quds Razavi inapanga kufanya vipindi vingine mbalimbali katika mnasaba huo adhimu.

Idadi kubwa ya mahujaji wanatarajiwa kuzuru kaburi takatifu la Imam Ridha (AS) huko Mashhad katika siku zijazo.

Siku ya 11 ya mwezi wa Hijri wa Dhu al-Qa’dah ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ridha (AS).

Mwaka huu, Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iran na kwingineko duniani watasherehekea sikukuu hiyo siku ya Jumatatu, Mei 20.

3488373

Habari zinazohusiana
captcha