Kwa mujibu wa Katibu wa shirika hilo, Seyyed Jalal Hosseini, "Tamasha hili lilifanyika hapo awali mnamo 2010, na mji wa Hamedan (magharibi mwa Iran) ulikuwa mwenyeji wa duru ya kwanza na ya pili. Kuanzia raundi ya tatu na kuendelea, Mashhad imekuwa ikiandaa tamasha hilo kutokana na uwezo wa taasisi ya Haram ya Imam Ridha (AS)
"Kwa ujumla, kazi 3,745 zimewasilishwa kwa sekretarieti katika duru zote zilizopita, ambapo kulikuwa na vitabu 410 vya Kiajemi na vingine katika lugha nyinginezo katika duru ya 13," aliongeza katibu huyo.
Akisisitiza kwamba duru inayokuja italenga kuongeza idadi na ubora wa tamasha hilo, Hosseini alisema: "Lengo kuu la tamasha la 14 ni kupanua shughuli za kisayansi, kitamaduni, utafiti, fasihi na kisanii kuhusu maisha na mwenendo wa Imam Reza.”
Awamu hii ya tukio ina mada kuu nane zikiwemo 'Hadith na Usimulizi', 'Maadili na Sayansi , Fiqhi ya Kiislamu na Sharia', 'Falsafa na Thiolojia, 'Saikolojia', Sayansi za Jamii, 'Wasifu, Historian a Anthropolojia' na 'Sayansi ya Tiba ya Imam Ridha: Mbinu za Zamani na Mpya'.
Sehemu ya kimataifa ya tamasha inaonyesha vitabu vilivyouzwa na wachapishaji wasio Wairani katika lugha tofauti.
"Sehemu mpya inayoitwa 'Mtumishi wa Fikra Razawi' imeongezwa hivi karibuni kwenye tamasha, ambayo inathamini waandishi na wachapishaji wa vitabu bora zaidi kuhusu Imam Ridha (AS) katika raundi tatu za tamasha", aliendelea kufafanuaHosseini.
Kwa mujibu wa Hujjatul Isalm Ali Bagheri, katibu wa kisayansi wa tamasha hilo, wahadhiri na wasomi waliobobea kutoka vyuo vya Kiislamu (Hauza) na vyuo vikuu vya juu nchini Iran wanaunda kamati na jopo la kisayansi.
3488567