Maimamu wa Georgia, wanaharakati wa Utamaduni wamtembelea Haram ya Imam Ridha (AS)
IQNA - Kundi la maimamu wa Swala ya Ijumaa na wanaharakati vijana wa kitamaduni kutoka Georgia walifanya ziara katika kaburi la Imam Ridha (AS) katika mji wa kaskazini mashariki mwa Iran wa Mashhad na kufanya mazungumzo na mkuu wa masuala ya kimataifa wa idara ya usimamizi wa eneo hilo takatifu.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Tousi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu tarehe 27 Mei, Hujjatul Islam Mostafa Faghih Esfandiari alisema: "Georgia na nchi nyingine za Asia ya Kati huzungumza kwa lugha yao ya asili na Kirusi. Hii ni fursa nzuri na vyombo vya habari kukuza mafundisho ya Kiislamu".
Aidha amewanasihi kwa kusema: “Tunatakiwa kuendelea na njia ya Imam Mahdi kifikra na kivitendo. Kwa ajili hiyo, ni lazima tuanze kujiboresha, ufahamu na kujifunza mafundisho ya Qur'an ili tuweze kuongeza uelewa wetu".
Pia amewataka vijana kujizatiti na imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu ili kukabiliana na maadui katika vita laini vinavyoibuka duniani.
Mwishoni mwa mkutano huo, Esfandiari alitoa wito kwa msafara wa watu wa Georgia kufanya kila wawezalo kuwaalika watu wengi zaidi kwenye Uislamu hadi mwaka ujao.
3488568