Mostafa Feizi, naibu mkuu wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Ridha (AS) ambayo ni maarufu kama Astan Quds Razavi, amesema mji huo uko tayari kuwapokea mahujaji.
Manispaa ya Mashhad, Idara ya Masuala ya Awqaf na Misaada, Idara ya Itikadi ya Kiislamu na mashirika mengine yanayohusiana yanatekeleza mipango ya kuwahudumia wafanyaziara au Zuwar, alisema.
Amebainisha kuwa kuongezeka kwa idadi ya wafanyaziara kunatokea minasaba mitatu ya siku za mwisho za mwezi wa Hijri wa Safar.
Kuna Mawkib 150 (vibanda vya kutoa vyakula, malazi na huduma kwa wafanyaziara) vimeanzishwa karibu na eneo hilo takatifu, kulingana na afisa huyo.
Feizi aidha amesema, Astan Quds Razavi imetayarisha programu mbalimbali za kidini na kitamaduni kwa ajili ya wafanyazaira katika siku kumi za mwisho za Safar, zikiwemo duru za kusoma Qur'ani na shughuli nyinginezo za Qur'ani, hotuba za kidini, ibada za maombolezo na mashindano ya usomaji wa vitabu.
Siku ya 28 ya Safar, ambayo ni Jumatatu, Septemba 2, ni kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Imam Hassan (AS). Siku ya 30 ya mwezi wa mwandamo, Septemba 4 mwaka huu, inaadhimishwa kama kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Ridha (AS), Imam wa nane wa Waislamu wa amdhehebu ya Shia.
3489696