Hujjatul Islam Ali Askari, naibu mkuu wa makao makuu ya huduma za usafiri za Mkoa wa Khorasan Razavi, amesema idadi ya wasafiri waliowasili Mashhad kutoka Agosti 14 hadi 23 ni 5,241,878.
Kati yao, 116,517 walifika kwa ndege, 181,140 kwa treni, 209,921 kwa usafiri wa umma barabarani, 4,189,395 kwa magari ya binafsi, na 545,030 kwa miguu, aliongeza.
Siku za mwisho za mwezi wa Hijri Safar ni nyakati za huzuni ambazo huadhimishwa kwa ibada za maombolezo nchini Iran na nchi nyingine.
Siku ya 28 ya Safar, iliyokuwa Ijumaa, Agosti 22, ni kumbukumbu ya kifo cha Mtume Mtukufu (SAW) na kumbukumbu ya shahada ya Imam Hassan (AS).
Siku ya 30 ya mwezi wa Safar, iloyokuwa Agosti 24 mwaka huu, huadhimishwa kama kumbukumbu ya shahada ya Imam Ridha (AS), Imam wa nane wa Kishia.
Kila mwaka katika siku hii, waumini wengi hutembelea kaburi la Imam Reza (AS) katika mji Mashhad.
3494374