IQNA

Uzinduzi wa Tarjuma ya Sauti ya Qur’ani kwa Lugha ya Kitajiki

17:42 - June 12, 2026
Habari ID: 3482350
IQNA – Maana ya aya za Qur’ani Tukufu sasa imeweza kufikika kwa wasikilizaji wanaozungumza Kitajiki kote duniani kupitia uzinduzi wa tarjuma ya sauti kwa lugha hiyo.

Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji wa Qur'ani Tukufu kimezindua tafsiri ya sauti ya maana ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kitajiki kupitia tovuti yake rasmi.

Hatua hii ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za kituo hicho kutumia teknolojia za kisasa katika kuhudumia Qur’ani Tukufu na kurahisisha upatikanaji wa tarjuma na tafsiri kwa Waislamu duniani wanaozungumza lugha mbalimbali.

Kituo hicho kimeeleza kuwa huduma hiyo inawawezesha watumiaji kusikiliza tarjuma ya sauti kwa Kitajiki, kuvinjari baina ya sura na aya, pamoja na kupakua faili za sauti.

Tarjuma hiyo ya sauti imeandaliwa kwa rekodi zenye ubora wa hali ya juu, usomaji ulio wazi, na uwasilishaji sahihi wa maana za aya za Qur’ani, jambo linalochangia kuongeza uelewa wa Qur’ani Tukufu miongoni mwa wazungumzaji wa Kitajiki.

Kituo cha Mfalme Fahd cha Uchapishaji wa Qur’ani Tukufu kipo katika mji mtukufu wa Madina.

Kila mwaka huzalisha mamilioni ya nakala za Msahafu wa Qur’ani Tukufu.

Pia huchapisha tafsiri na tarjuma za Kitabu Kitukufu hicho katika lugha mbalimbali.

3497808

captcha