IQNA

Meya Mwislamu wa New York apinga sera za Trump za kuwabana wageni wakati wa Kombe la Dunia

17:29 - June 10, 2026
Habari ID: 3482345
IQNA – Meya Mwislamu wa Jiji la New York, Zohran Mamdani, siku ya Jumatano alipinga vikali mipango ya utawala wa Trump ya kuongeza uwepo wa maafisa wa Idara ya Uhamiaji, kwa kifupi ICE, jijini humo wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia.

Amesema kuwa mpango wa utawala wa Trump wa kuongeza idadi ya maafisa wa ICE katika jiji hilo “utaharibu roho na hamasa ya Kombe la Dunia.”

Tom Homan, anayesimamia masuala ya mipaka katika utawala wa Donald Trump, akizungumza kupitia Fox News siku ya Jumatatu, alisema: “Mtaona uwepo wa ICE kwa kiwango ambacho hamjawahi kukiona hapo kabla katika Jiji la New York, na hilo linakuja. Nimepitia tayari mpango wa operesheni.”

Kombe la Dunia linatarajiwa kuvutia maelfu ya wageni kutoka mataifa mbalimbali katika eneo la New York na vitongoji vyake, ambalo litakuwa mwenyeji wa mechi kadhaa, ikiwemo fainali.

Meya Mwislamu wa New York apinga sera za Trump za kuwabana wageni wakati wa Kombe la Dunia

Mamdani, katika ujumbe wake aliouchapisha kwenye jukwaa la X, aliandika:

“Soka isingekuwepo bila ya wahamiaji. Wahamiaji ndio wanaocheza na kufundisha mchezo huu, wanafanya kazi viwanjani, wanajaza majukwaa, na wanafanya sherehe kama Kombe la Dunia ziwezekane. Wachezaji sita wa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani ni wahamiaji. Haturuhusu ICE wala yeyote mwingine kupanda hofu katika jamii zetu,hasa katika wakati kama huu. Dunia inapokuja katika jiji letu, sisi tutasimama kwa fahari pamoja na majirani zetu wahamiaji na tutakataa mashambulizi haya kwa hakika yake yalivyo: ni jaribio la kutugawa.”

3497776

Habari zinazohusiana
captcha