IQNA

17:10 - February 03, 2020
News ID: 3472437
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mkubwa zaidi katika eneo la Asia ya Kati uliojengwa katika mji mkuu wa Tajikistan, Dushanbe, utafungulwia rasmi mwezi ujao wa machi.

Msikiti huo ulikuwa umepengwa kufunguliwa rasmi Oktoba 2019 na Emir wa Qatar, lakini safari yake nchini Tajikistan iliahirishwa hadi Machi 2020.

Msikiti huo wa aina yake una uwezo wa kubeba watu 120,00 na umejengwa na wataalamu wa Tajikistan na Qatar.  Msikiti huo uliojengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 12 pia una maktaba, jengo la makumbusho, ukumbi wa mikutano na ukumbi wa maamkuli. Ujenzi wa msikiti huo ulianza Oktoba 2009 na unakadiriwa kugharimu dola milioni 100. Taarifa zinasema Qatar imegharamia kikamilifu ujenzi wa msikiti huo.

Tajikistan ni nchi ndogo ya Asia ya Kati ambayo haina pwani kwenye bahari yoyote. Imepakana na Uchina, Afghanistan, Uzbekistan na Kyrgyzstan na idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 9.2 ambapo asilimia 97 ya raia wake ni Waislamu.

Mwaka 1868 Tajikistan ilivamiwa na Urusi na kuwa sehemu ya Dola la Urusi, halafu sehemu ya Umoja wa Kisovyet baada ya mapinduzi ya 1917. Iliitwa Jamhuri ya Kisovyet ya Kisoshalisti ya Tajikistan. Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoviet, Tajikistan ilipata uhuru wake mwaka 1991.

3876228

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: