IQNA

Manispaa ya Tehran Yakamilisha Maandalizi ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi

11:48 - June 09, 2026
Habari ID: 3482342
IQNA – Msemaji wa Manispaa ya Tehran ametangaza utayari kamili wa manispaa hiyo kwa ajili ya shughuli ya kusindikiza mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Abdolmotahhar Mohammadkhani aliyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu, Juni 8 jijini Tehran.

Akibainisha mipango ya hafla ya mazishi ya kiongozi huyo shahidi, Mohammadkhani alisema Manispaa ya Tehran inajiandaa kufanya mazishi ya kihistoria kwa ajili ya Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei. “Tunatumai kuwa tutaweza kutoa huduma bora katika eneo hili,” alieleza.

Kwa mujibu wa maafisa, shughuli za kusindikiza mwili wa Kiongozi huyo Shahidi zitafanyika mjini Tehran pamoja na miji mitukufu ya Qom na Mashhad.

Imam Khamenei, akiwa pamoja na idadi ya makamanda waandamizi na maafisa wa Iran, alifikia daraja ya shahidi kufuatia shambulio la anga la kigaidi la Marekani na utawala wa Israel dhidi ya ofisi yake mjini Tehran mnamo 10 Ramadhani 1447 sawa na Februari 28, 2026.

Katika kujibu uvamizi huo wa Marekani na Israel ulioendelea kwa siku 40, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitekeleza Operesheni ya “Ahadi ya Kweli ya Nne” , iliyojumuisha mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (drones) dhidi ya malengo ya Israel na vituo vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi.

3497763

captcha