IQNA

Rais Raisi: Jumuiya ya Shanghai inaweza kuwa tegemeo la kiuchumi na kisiasa

20:42 - September 17, 2021
Habari ID: 3474307
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inaweza kuwa kichocheo muhimu cha mtazamo mmoja wa pande kadhaa ulimwenguni.

Rais Ibrahim Raisi amesema hayo katika hotuba yake leo kwenye mkutano wa 21 wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai huko Dushanbe mji mkuu wa Tajikistan na kueleza kwamba, jumuiya hiyo imeonyesha vizuri kwamba, inaweza kugeuka na kuwa tegermeo la kiuchumi na kisiasa katika mtazamo mmoja na ushirikiano wa kadhaa ulimwenguni.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, sera za kigeni za Tehran siku zote zimejikita katika ushiriki amilifu katika asasi na jumuiya za kimataifa, mitazamo ya pande kadhaa na kupinga uchukuaji maamuzi wa upande mmoja.

Aidha Sayyid Ibrahim Raisi amesema katika hotuba yake hiyo kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikitilia mkazo suala la ushirikiano uliojengeka katika msingi wa kuheshimiana na udharura wa kuweko mchango wenye kujenga kwa minajili ya kukabiliana na changamoto za kieneo na kimataifa.

Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai ulianza Alkhamisi ya jana katika mji mkuu wa Tajikistan Dushanbe, ambapo Rais Ibrahim Raisi ameuongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkutano huo, hii ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipoapishwa na kuwa rais mwezi Agosti.

Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai iliasisiwa mwaka 2001 kwa lengo la kukabiliana na ugaidi na vitendo vya uchupaji mipaka na kuimarisha ushirikiana wa kiuchumi. Wanachama wa sasa wa jumuiya hiyo ni pamoja na China, India, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Russia, Pakistan, Tajikistan, and Uzbekistan;  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Afghanistan, Belarus na Mongolia ni wanachama watazamaji katika jumuiya hiyo. Inatazamiwa kuwa Iran itajiunga rasmi kama mwanachama  kamili wa SCO siku za usoni.

131318

Kishikizo: iran ، rais raisi ، Shanghai ، SCO ، Tajikistan
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha