IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Shahidi Qassem Soleimani alileta amani endelevu kupitia mapambano (muqawama)

19:49 - January 10, 2020
Habari ID: 3472358
TEHRAN (IQNA) - Katibu wa sala ya Ijumaa mjini Tehran amemtaja shahidi Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kuwa ni mratibu wa usalama na amani endelevu kupitia mapambano (muqawama).

Hujjatul Islam Mohammad Javad Haj Ali Akbari, hatibu wa muda wa sala ya Ijumaa mjini Tehran sambamba na kuashiria kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, amesema kuwa wiki iliyopita anga ya Iran, eneo la Asia Magharibi na nchi zote za Kiislamu iligubikwa na kumcha-Mungu. Akibainisha sifa za kipekee za Jenerali Soleimani katika kumcha Mwenyezi Mungu ameongeza kwamba, shakhsia huyo mwenye daraja ya juu aliwasambaratisha magaidi wa Daesh (ISIS) na kuimarisha usalama katika eneo la Asia Magharibi sambamba na kupanua utamadunia wa muqawama katika ngazi ya kieneo. Hatibu wa sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo mjini Tehran amebainisha kwamba, upana wa stratijia za Luteni Soleimani katika uwanja wa muqawama, umedhamini usalama wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama ambavyo pia umedhamini hata usalama wa dunia, usala ambao umepatikana kutokana na harakati za kimuqawama. 

Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema kuwa kwa kufuata nyendo za Imam Khomeini (MA), Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alifanya juhudi kubwa katika kuwalea vijana kiimani, kishujaa, kuwa na fikra chanya na mtazamo wa kiutamaduni katika eneo pana la kimuqawama na kupanua pia utamaduni wa malezi ya Uislamu asilia katika eneo. Ameendelea kubainisha kwamba Wamarekani walifanya ujinga mkubwa kwa kumuua shahidi Luteni Qassem Soleimani na kusema kuwa, kumuua kigaidi shakhsia huyo pamoja na marafiki wake, kumeamsha hisia za mwono wa umma wa Kiislamu, kuwaunganisha pamoja wananchi, kuunda anga ya upole katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na katika eneo la muqawama.

3870494/

captcha