IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
13:01 - January 08, 2020
News ID: 3472353
TEHRAN (IQNA) -Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mashambulio ya makombora yaliyofanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC katika kambi mbili za Marekani nchini Iraq ni kibao cha uso tu alichopigwa adui huyo.

Amesema, majibu ya Iran hayatoishia hapo kwani kinachotakiwa hasa ni kuangamizwa kikamilifu uwepo wa kifisadi na kiharibifu wa Marekani katika eneo hili zima.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo asubuhi (Jumatano) wakati alipoonana na maelfu ya wananchi wa Qum na huku akitilia mkazo uhakika kwamba mataifa ya eneo hili na tawala zilizotokana na wananchi, bila ya shaka yoyote hazitaki kuona Marekani inaendelea kuwepo katika eneo lao, amesema, kuwepo Wamarekani kwenye eneo hili na katika sehemu yoyote ile duniani hakuna matokeo mengine isipokuwa vita, ugomvi, fitna na kuharibiwa miundombinu ya eneo hilo.

Vile vile amezungumzia nafasi ya kipekee isiyo na mbadala ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani katika kufelisha njama za Marekani huko Palestina, Iraq na Lebanon na kuongeza kuwa, shahid Luteni Jenerali Soleimani alifanikiwa kuvunja na kufelisha njama zote za Marekani zilizotumia fedha nyingi, mabavu, uchochezi wa kisiasa na uundaji wa makundi mbalimbali.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, tunaposema "adui" tunakusudia Marekani, utawala wa Kizayuni na majimui ya vibaraka wao na kuongeza kuwa, baadhi ya tawala za ndani na nje ya eneo hili hazipaswi kuingizwa kwenye kundi hilo la adui hadi pale zitakapochukua hatua ya kumtumikia adui.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesisitiza kuwa, muswada uliopasishwa na bunge la Iraq wa kufukuzwa wanajeshi wa Marekani nchini humo ni hatua nzuri sana na tunamuomba Mwenyezi Mungu alete taufiki ya kuendelea jambo hilo katika nchi nyinginezo.

Aidha Kiongozi Muadhamu amesema: "Kile ambacho ni muhimu ni kuwa hatua kama hiyo ya kijeshi tuliyochukua haitoshi katika kadhia hiyo, kile ambacho ni muhimu ni kuwa, uwepo wa Marekani wenye kuibua ufisadi katika eneo ufike ukingoni. Wameleta vita katika eneo hili, wameleta hifilafu na fitina, wameleta uharibifu, wameharibu miundo msingi. Na hilo si katika eneo lete tu bali ni kila mahala amabpo Wamarekani wameweka mguu wao duniani."

3870172

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: