IQNA

Rais Hassan Rouhani
18:28 - January 08, 2020
News ID: 3472354
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia majibu makali yaliyotolewa usiku wa kuamkia leo na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC ya kuwashambulia magaidi wa Kimarekani katika kambi zao mbili za kijeshi nchini Iraq na kusema kuwa, majibu kamili ya Iran kwa jinai za Wamarekani ni kukatwa miguu yao kwenye eneo hili.

Rais Rouhani amesema hayo kwenye kikao cha leo cha Baraza la Mawaziri na kusisitiza kuwa, jinai ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC na wanamapambano wenzake huko Iraq, usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020, ni ukiukaji wa sheria zote za kimataifa, ni jinai ya kivita na ni ugaidi wa kimataifa. Ameongeza kuwa, Marekani imeshindwa kufikia malengo yake kwenye jinai yake hiyo.

Vile vile amesema, Marekani imefanya kosa kubwa sana la kihistoria na kusisitiza kwamba, Kamanda Soleimani hakuwa kamanda wa kijeshi tu, bali alikuwa mwanasiasa, mwanastratijia na mtu madhubuti katika mazungumzo ya kisiasa na vyama, makundi na hata viongozi wa ngazi za juu wa eneo hili na wa nje ya eneo hili.

Rais Rouhani pia amesema, Marekani ndiye mbeba dhima mkuu wa jinai hiyo na inabibi ayape majibu mataifa ya eneo hili ya kwa nini amefanya jinai kama hiyo. 

Vile vile ameonya kwamba, kama kuanzia sasa Marekani itaamua kufanya jinai nyingine yoyote, basi itambue kuwa itapata majibu makali zaidi ya iliyopata usiku wa kuamkia leo.

Itakumbukwa kuwa, usiku wa kuamkia leo Jumatano, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC limezipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyiofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

Rais Rouhani ametoa shukrani za dhati kwa IRGC kwa kusema: "Sisi tunatoa shukurani kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa kutekeleza oparesheni hiyo dhidi yay a kituo kikubwa cha akijeshi cha Marekani katika eneo. Oparesheni hiyo inaonyesha hatuawezi kulegeza msimamo mkabala wa Marekani. Kwa hivyo Marekani ifahamu kuwa, ikitenda jinai ifahamu kuwa itapokea jibu kali kutoka Iran na tayari imeshapokea jibu"

3870251

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: