IQNA

Khitma ya kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Soleimani na wanamapambano wenzake

17:53 - January 09, 2020
Habari ID: 3472355
TEHRAN (IQNA) -Khitma kwa mnasaba wa kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wanajihadi wenzake katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mefanyika leo hapa Tehran katika Husseiniya ya Imam Khomeini kwa kuhudhuriwa na Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ambaye Ijumaa alfajiri iliyopita (3 Januari 2019) alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo; aliuliwa shahidi siku hiyo hiyo akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis Naibu Mkuu wa harakati ya al Hashd al Shaabi na wenzao wanane katika shambulio la anga la wanajeshi vamizi na magaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad. 

Khitma ya Shahidi Luteni Jenerali Shujaa Qassem Soleimani, mwanajihadi mkubwa Abu Mahdi Al Muhandis na mashahidi wengine nane imehudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Rais Hassan Rouhani, makamanda wa ngazi za juu wa kijehsi na wawakilishi wan chi kadhaa za kigeni pamoja na maelefu ya wananchi.

Khitma hiyo pia imehutubiwa na Mkuu wa kundi la al Hashd al Shaabi la Iraq ambaye ametoa mkono wa taazia kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wa Iran kufuatia kuuliwa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani. Falih al Fayyadh amesema: Ni hali ngumu sana kwa Iraq kuona damu safi ya wapendwa hao imemwagwa huko Iraq yaani katika ardhi ya Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein AS.

Mkuu wa Harakati ya al Hashd al Shaabi ya Iraq amesema katika marasimu hayo yaliyohudhuriwa pia na wakuu wa mihimili mitatu ya dola, maafisa wa jeshi na wa serikali ya Iran na Iraq, wawakilishi wa makundi ya muqawama na mabalozi wa nchi za nje kwamba: Wananchi wa Iraq wako imara kwa pamoja kutokana na majonzi ya kumpoteza Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la IRGC na wametangaza kuunga mkono harakati za shahidi Soleimani.

Amemuomboleza pia shahidi Abu Mahdi al Muhandis na kueleza kuwa: Shahidi Abu Mahdi alikuwa bega kwa bega pamoja na Shahidi Soleimani na wanamapambano wenzao katika vita dhidi ya utakfiri na kwa ajili ya kudhamini amani na uthabiti kwa wananchi wa Iraq; na hatimaye pia nyama na damu za mashahidi hao wawili zimechanganyika pamoja. 

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Jumatano alfajiri lilijibu ugaidi wa Marekani wa kumuua Luiteni Jenerali Qassem Soleimani na wenzake kwa kuvurumisha makumi ya makombora katika kambi za Marekani zilizoko katika mikoa ya al Anbar na Arbil huko Iraq.    

3870387

captcha