IQNA

18:55 - January 14, 2020
News ID: 3472372
TEHRAN (IQNA) – Mwenyekiti wa Baraza la Kiislamu Malaysia (MAPIM) amesema hatua ya Marekani ya kumuua kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Luteni Jenerali Qassem Soleimani ni ugaidi wa kiserikali na ukweli wa mambo ni kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ni muuaji.

Katika kikao kilichofanyika Shah Alam nchini Malaysia, Jumanne, mwenyekiti wa MAPIM Sheikh Mohammad Azmi Abdul Hamid amesema askari wote wa Marekani wanapaswa kuondoka Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) bila masharti. Aidha ametoa wito wa kufikishwa Marekani katika katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa kutenda jinai za kivita dhidi ya Iran. Kikao hicho kiliitishwa kwa lengo la kujadili ugaidi wa Marekani dhidi ya Iran.

Washiriki wa kongamano hilo wamesema utawala haramu wa Israel ndio unaofaidika na migogoro yote inayoibuliwa na Marekani eneo la Asia Magharibi. Aidha wamesema kinyume cha madai ya utawala wenye misimam mikali wa Trump kuwa eti Iran ni tishio kwa dunia, utawala haramu wa Israel ndio tishio kuu kwa usalama wa dunia.

Halikadhalika wamesema mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani mapema Januari 3 2020 ni sawa na mauaji ya Archduke Ferdinand wa Austria mano Juni 1914, mauaji ambayo yaliibua vita vya kwanza vya dunia.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine nane, walishambuliwa na ndege zisizo na robani za jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote walikufa shahidi katika tukio hilo.

Kufuatia ugaidi huo wa Marekani usiku wa kuamkia Jumatano 8 Januari, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC lilizipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyiofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

3470363

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: