IQNA

Madrassah za Qur'ani zafungwa Oman na Morocco kutokana na hofu ya corona

19:09 - March 15, 2020
Habari ID: 3472569
TEHRAN (IQNA)- Madrassah zote za Qur'ani zimefungwa kwa muda Morocco na Oman kutokana na hofu ya kuoena ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona.

Kwa mujibu wa tovuti ya shuoon.om Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Oman imetangaza kuwa madrassah zote za Qur'ani zinazofungamana na wizara hiyo zimefungwa.

Taarifa hiyo imesema, hatahivo masomo ya Qur'ani yataendelea kwa njia ya intaneti. Hatua hizo zimechukuliwa kufuatia hatua ya awali ya kufunga shule na vyuo vikuu nchini humo.

Nchini Morocco, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nayo imetangaza kufunga kwa muda shule, vyuo vikuu na madrassah za Qur'ani kwa lengo la kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID 19.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, hadi kufikia leo, watu waliokuwa wameambukizwa COVID-19 kote duniani wamepindukia 152,428 huku waliofariki wakiwa ni zaidi ya 5,720 katika nchi 141 kote duniani.

3885423

captcha