IQNA

Sala ya Ijumaa haikusaliwa misikiti kadhaa Marekani kutokana na hofu ya corona

11:46 - March 14, 2020
Habari ID: 3472563
TEHRAN (IQNA) – Sala ya Ijumaa haikusaliwa katika misikiti kadhaa nchini Marekani kutokana na hofua ya kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona

Jumuiya ya Waislamu ya Eneo la Dulles (ADAM) ilishauri sala ya Ijumaa isisaliwa katika misikiti 10 iliyo chini ya usimamizi wake na waumini walishauriwa wasalia maeneo waliko.

Nao msikiti wa Dar al-Hijrah ambao ni kati ya misikiti mikubwa Virginia nao pia ulitangaza kuwa sala ya Ijumaa haitasaliwa na kubatilisaha uamuzi wake wa awali wa kuwaruhusu waumini 400 pekee.

Baraza la Maimamu la Michigan, ambalo huwaleta pamoja maimamu wa Kishia na Kisunni, nalo pia lilitangaza kuwa sala ya Ijumaa haitasaliwa katika eneo hilo kufuatia ushauri wa wataalamu wa tiba.

Viongozi wa Kiislamu Marekani wanasema wanawasiwasi kuhusu hali itakavyokuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati  Waislamu hujumuika pamoja kwa ajili ya ibada.

Jumuiya ya Kitiba ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini na Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini zimetoa taarifa ya pamoja na kusema lengo la kusitisha kwa muda sala za jamaa na sala ya Ijumaa ni kulinda maisha ya waumini. Taarifa hiyo imesema kulinda maisha ya mwandamu ni singi muhimu wa sheria za Kiislamu. Hadi kufikia sasa watu watu 2,174 wameambukizwa corona nchini Marekani huku 48 miongoni mwao wakifariki.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, wataalamu wanasema watu kati ya milioni 160 hadi milioni 214 wanaweza kuambukizwa corona nchini Marekani. Wataalamu hao wanasema maambukizi yanaweza kuendelea hadi mwaka moja na kwamba watu baina ya 200,000 na milioni 1.7 wanaweza kufariki.

3470903

captcha