Kwa mujibu wa waziri anayeshughulikia masuala ya kidini Dr. Zulkifli Mohammad al-Bakri, “shughuli zote za misikiti, ikiwa ni pamoja na sala ya Ijumaa na sala za jamaa zimesimamishwa kwa muda kuanzia Machi 17 hadi 26.” Amesema wamechukua uamuzi huo kufuatia ushauri wa wizara ya afya. Amesema kwa mujibu wa ushauri wa mwaka 2015 wa Kamati ya Fatwa, iwapo Muislamu nchini humo atafariki kutokana na COVID-19 mwili tayammum itafanywa juu ya mfuko uliko mwili.
Hadi sasa kuna watu 553 waliomabukizwa corona nchini Malaysia na miognoni mwao mtu moja, aliyekuwa na umri wa miaka 60, amefariki.
3470935