IQNA

15:07 - March 12, 2020
News ID: 3472557
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Masuala ya Kiislamu katika ufalme wa Saudi Arabia ameamuru kuwa sala ya Ijumaa katika misikiti nchini humo isizidi dakika 15.

Amri hiyo ni kati ya hatua ambazo zimechukuliwa kwa muda kuhusu sala ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona nchini humo.

Kwa mujibu ya amri ya Waziri wa Masuala ya Kiislamu Saudia wakati baina ya adhana ya kwanza na  adhana ya pili katika sala ya Ijumaa ni dakika 10 katika misikiti yote ya ufalme huo. Taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wa Twitter wa waizara hiyo imesema, waziri pia amesema kuwa muda jumla wa Sala ya Ijumaa usizidi dakika 15.

Aidha Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudia imesema misikiti imetakiwa kutoandaa futari na itikaf.

Wizara ya Afya ya Saudia imesema kwa ujumla kuna watu 20 ambao wameambukizwa kirusi cha Corona katika ufalme huo.

3470871

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: