IQNA

14:25 - March 12, 2020
News ID: 3472556
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Malaysia ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika mwezi Aprili sasa yameakhirishwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama corona.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,  mashindano hayo yanatazamiwa kufanyika mwezi Juali mwaka huu wa 2020.  Wanaoandaa mashindano hayo  wamesema shughuli zote za kiutamaduni zimeakhirishwa nchini Malayasia ili kuzuia kuenea kirusi cha corona na kwa msingi huo, mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nayo pia yameakhirishwa. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa kufanyika mashindano hayo mwezi Julai pia kutategemea hali ya mambo wakati huo kuhusu vita dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Shirika la Afya Duniani jana Jumatano limetangaza kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeenea kote duniani ambapo kuna wagonjwa 118,000 katika mataifa 114 ambapo tayari watu 4,291 wamefariki dunia.

3884880

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: