Sayyid al Qubanchi ambaye alikuwa akihutubia waumini katika swala ya Ijumaa amesema kuwa katika siku ya Ashura yaani tarehe 10 Muharram, Waislamu hutangaza tena utiifu wao kwa malengo ya harakati na njia ya Imam Hussein (as).
Ameongeza kuwa kila mtu anayetaka izza, heshima, uhuru na kutokomezwa utawala wa Kizayuni wa Israel anapaswa kuhuisha jina la Imam Hussein kwani jina na wito wa mtukufu huyo umekomboa mataifa mbalimbali.
Imam wa swala ya Ijumaa ya Najaf pia amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyowalenga waombolezaji wa mauaji ya Imam Hussein (as) katika miji ya Baghdad na Diali huko Iraq na Chabahar nchini Iran.
Vilevile amewashukuru Waislamu katika nchi mbalimbali duniani kwa kushiriki kwa wingi katika shughuli za maombolezo ya tukio chungu la kuuawa mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as). 713547