IQNA

Sayyid Hassan Nasrullah ahudhuria maombolezo ya Imam Hussein (as)

16:09 - December 07, 2011
Habari ID: 2234734
Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon jana Jumanne alihudhuria maombolezo ya Ashura katika mwezi wa Muharram ambayo ni siku aliyouawa shahidi Imam Hussein bin Ali bin Abi Twalib (as), mkujuu wa Mtume Mtukufu (saw).
Akizungumza katika maombolezo hayo yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji wa Lebanon katika uwanja wa michezo wa ar-Rayya kusini mwa Beirut, Sayyid Nasrullah amesema kuwa alikuwa na hamu kubwa ya kujiunga na waombolezaji hao ili kwa pamoja wautangazie ulimwengu wote azma na baia yao mpya kwa Imam Hussein (as) ambaye alisimama pekee yake na kwa ushupavu mkubwa mbele ya jeshi la watu 30,000, maadui wa Uislamu.
Kiongozi wa Hizbullah alisema, katika kipindi hicho Imam Hussein (as) alilazimika kuchagua chaguo moja kati ya mawili ya ama kupigana na kutetea dini ya Mwenyezi Mungu au kujidhalilisha kwa kukubali matakwa ya maadui wa dini. Sayyid Nasrullah alisema wao ni wafuasi wa Imam Hussein (as) ambao wamechagua nara ya kutokubali udhalilifu mbele ya maadui wa dini.
Hayo yalikuwa mahudhurio ya kwanza na ya moja kwa moja ya Nasrullah hadharani mbele ya umati mkubwa wa watu tokea mwaka 2008. 911275
captcha