
Mashabiki wake walisambaza picha na video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 akiwa amebeba bendera ya Palestina uwanjani.
Bouy amekuwa miongoni mwa wachezaji mashuhuri zaidi wa Galatasaray katika miaka ya hivi karibuni akicheza nafasi ya beki wa kulia. Hapo awali aliwahi pia kuchezea klabu ya Bayern Munich.
Hatua yake ya kuonesha mshikamano na Palestina imekuja siku chache baada ya tukio linalofanana na hilo kufanywa na nyota chipukizi wa timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal, ambaye naye alionekana akibeba bendera ya Palestina mabegani mwake wakati wa sherehe za ubingwa wa Ligi ya Hispania za Barcelona.
Yamal alikabiliwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa vyombo vya habari vya utawala katili wa Israel na baadhi ya maafisa wake kufuatia kitendo hicho, lakini wakati huohuo alipokea pongezi nyingi kutoka kwa vyombo vya habari na hata waziri mkuu wa Hispania, ambaye alitetea kwa nguvu msimamo wa mchezaji huyo kijana.
Hii si mara ya kwanza kwa bendera ya Palestina kuonekana katika sherehe za Galatasaray.
Miaka miwili iliyopita, nyota wa Morocco, Hakim Ziyech, alijifunika kwa bendera ya Palestina wakati wa sherehe za ubingwa wa Ligi ya Uturuki za timu hiyo, katika kipindi ambacho utawala wa Israel ulikuwa ukiendelea na vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza.
3497492