IQNA

Juhudi mpya za kuwaelimisha Mahujaji kuhusu adabu za Msikiti wa Mtume

17:18 - May 18, 2026
Habari ID: 3482253
IQNA – Juhudi mpya za kuimarisha uelimishaji na uhamasishaji zimetangazwa ili kuwasaidia mahujaji na wageni waelewe vyema adabu za kuingia, kuswali na kutoa salamu kwa Mtume Muhammad (S.A.W.) katika Msikiti wa Mtume maarufu kama Al Masjid An Nabawi uliopo Madina.

Urais Mkuu wa Masuala ya Kidini katika Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume nchini Saudi Arabia umeimarisha juhudi za uelimishaji na uelekezaji kwa mahujaji na wageni, ili kuwafundisha adabu za kuzuru Al Masjid An Nabawi.

Juhudi hizi zinafanywa kupitia mfumo jumuishi wa nyenzo za mwongozo na maudhui yenye manufaa yanayowasilishwa kwa lugha mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha ufahamu wa kidini na kielimu wa wageni wakati wa msimu wa Hija.

Miongoni mwa programu za uhamasishaji ni utoaji wa maelekezo ya moja kwa moja ndani ya Al Masjid An Nabawi na katika viwanja vyake, pamoja na matumizi ya skrini za kidijitali, machapisho ya uelimishaji, na maudhui ya kidijitali ya lugha nyingi.

Programu hizi zinalenga kuwafahamisha Mahujaji kuhusu hukmu na adabu zinazohusiana na ziara hiyo, pamoja na kuhimiza mwenendo unaoonesha heshima na taadhima kwa mahali patakatifu, huku ukilinda utulivu na nidhamu ndani ya Al Masjid An Nabawi, taarifa hiyo iliongeza.

Urais huo pia umethibitisha dhamira yake ya kuwasilisha ujumbe wa uhamasishaji kwa njia zilizo rahisi kufikiwa, kwa kuzingatia tofauti za mataifa na lugha za Mahujaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha na kuboresha uzoefu wao wa kiroho.

3497491

captcha