Akizungumza siku ya Jumanne na wakuu wa tasisi na mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia masuala ya haki za binadamu nchini Lebanon katika majengo ya ubalozi huo, Balozi Rukn Abadi amesisitiza kuwa maslahi ya Wazayuni ndiyo yanayozuia kurejeshwa haki za taifa madhlumu la Palestina. Amesema kuwa pendekezo lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kutatuliwa mzozo wa Palestina ndiyo njia pekee ya kutatua mgogoro huo na matatizo mengine mengi yanayolikumba eneo la Mashariki ya Kati.
Balozi Rukn Abadi ameashiria mgogoro wa Syria pia na kusema kuwa Iran inashirikiana na viongozi wa nchi hiyo kwa lengo la kutekeleza matakwa ya waliowengi nchini humo na wakati huohuo kuunga mkono marekebisho ya kisiasa yanayofuatiliwa na Rais Bashar Asad.
Balozi Rukn Abadi amemaliza kwa kusema kuwa siasa za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimejengeka katika msingi wa katiba ya nchi inayounga mkono na kutetea thamani muhimu za kibinadamu kama vile haki, uadilifu na mapambano dhidi ya dhulma. 945107