Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qaf, vikao hivyo vya Qur'ani vimeandaliwa kwa munasaba wa maombolezo ya siku 10 za Muharram ambayo yanafanyika katika misikiti mbali mbali Kuwait.
Kati ya maqarii mashuhuri wa Kuwait watakaosoma Qur'ani katika vikao hivyo ni pamoja na Salih Al-Jahromi, Talal Al-Barik, Basil Bureza, Abbas Al-Baloushi, Sadiq Mirza, Hamdi Shibli, Zayd Al-Baqli, Muhammad Al-Mahdi na Abdullah Al-Khayyat.
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wale wote wanaowapenda Ahul Bayt AS wanashiriki katika vikao au majlisi za Muharram kote duniani.../mh