IQNA

Miaka tisa baada ya mauaji ya Msikiti wa Quebec, Waislamu wa Kanada watafuta haki

14:44 - January 30, 2026
Habari ID: 3481867
IQNA – Wakati kumbukumbu ya miaka tisa tangu shambulio la risasi katika msikiti wa Jiji la Quebec, Kanada (Canada) lililoua waumini sita waliokuwa katika ibada jamii za Kiislamu pamoja na washirika wao wanakusanyika si kwa ajili ya kukumbuka pekee, bali pia kutoa wito wa dharura.

Wanataka kukabiliwa na kuvunjwa kabisa kwa matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) ambayo bado yanaendelea kuchochea vurugu na hofu katika jamii.

Viongozi wa Kiislamu nchini Kanada wanatoa wito wa kusitishwa mara moja kwa lugha za kuchochea hofu na chuki dhidi ya Waislamu, wakisisitiza kuwa heshima, usalama na utu wa waumini ni haki ya msingi inayopaswa kulindwa kwa vitendo, si kwa maneno matupu.

Stephen Brown, Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Waislamu wa Kanada (NCCM), amesema kuwa kumbukumbu ya tukio la Alhamisi ni ukumbusho mzito kwamba chuki dhidi ya Uislamu nchini Kanada “si jambo dogo wala lisilo na madhara.”

“Ni jambo ambalo, kwa masikitiko makubwa, huua watu,” Brown aliliambia shirika la habari la Al Jazeera. “Kumbukumbu hii inatulazimisha kukumbuka kuwa chuki ina athari za kweli na zenye maumivu.”

Wanaume sita Waislamu waliuawa baada ya mshambuliaji kufyatua risasi katika Kituo cha Kiislamu cha Utamaduni cha Quebec (Quebec Islamic Cultural Centre) mjini Quebec mnamo Januari 29, 2017, tukio lililokuwa shambulio baya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya nyumba ya ibada katika historia ya Kanada.

Shambulio hilo liliacha jamii ya Waislamu wa Quebec ikiwa imetikisika kwa kina, likachochea mikusanyiko ya dua na mshikamano (vigils), pamoja na lawama kali kote Kanada, na pia likaangazia kwa uwazi ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu na msimamo mkali duniani kote.

Serikali ya Kanada ililaani tukio hilo kama “shambulio la kigaidi” lililolenga Waislamu, na ikaahidi kushughulikia mizizi ya matatizo yanayochochea chuki hiyo.

An event held to honor those killed in the Jan. 29, 2017, Quebec City mosque attack.

Mnamo mwaka 2021, ilitangaza Januari 29 kuwa ni Siku ya Kitaifa ya Kumbukumbu ya Shambulio la Msikiti wa Mji wa Quebec  na Hatua Dhidi ya Chuki ya Kiislamu (Islamophobia).

Hata hivyo, Brown amesema kuwa hana uhakika iwapo mafunzo yaliyopaswa kujifunzwa baada ya yaliyojiri Quebec  bado yanakumbukwa kikamilifu leo, karibu muongo mmoja baadaye.

Habari inayohusiana:

“Baada ya mauaji ya msikiti wa Quebec, kwa kweli kulikuwapo hamu ndani ya jamii kujaribu kutibu baadhi ya majeraha na kujenga madaraja ya uelewano,” alisema. “Kwa masikitiko, kile ambacho watu wengi wanashuhudia sasa, hasa Waislamu wanaoishi Quebec, ni kurejea kwa kiwango kikubwa kwa matumizi ya chuki dhidi ya Uislamu na kusambaza hofu ya Waislamu kwa maslahi ya kisiasa.”

Amira Elghawaby, mwakilishi maalum wa Kanada katika kupambana na chuki dhidi ya Uislamu, amesema serikali ya Kanada imeendelea kuonyesha dhamira ya dhati katika kukabiliana na tatizo hilo. Hatua hizo zinajumuisha Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Chuki (Action Plan on Combatting Hate) uliozinduliwa mwaka 2024, ambao umetenga mamilioni ya dola kwa makundi ya kijamii, programu za kupambana na ufashisti, na juhudi nyingine mbalimbali.

Hata hivyo, Elghawaby aliliambia Al Jazeera kuwa licha ya juhudi hizo, chuki dhidi ya Waislamu bado inaongezeka nchini Kanada, “iwe ni kupitia uhalifu wa chuki unaoripotiwa kwa polisi, au kupitia Wakanada wanaosema wanakumbana na ubaguzi mahali pa kazi na shuleni.”

Kwa mujibu wa Takwimu za Kanada (Statistics Canada), jumla ya matukio 211 ya uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu yaliripotiwa kwa polisi mwaka 2023, ongezeko la asilimia 102 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. 

Kulikuwa na ongezeko dogo zaidi mwaka 2024, ambao ni mwaka wa hivi karibuni zaidi wenye takwimu zilizopo, ambapo matukio 229 yaliripotiwa. 

3496227
captcha