IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Marekani inaeneza chuki dhidi ya Iran duniani

10:33 - April 28, 2016
Habari ID: 3470276
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema hatua ya Wamarekani ya kung'ang'ania kuiwekea vikwazo mbalimbali Iran ni njama za kueneza chuki na kulifanya taifa hili liogopwe na kwamba.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika hadhara ya maelfu ya wafanyakazi wa pembe mbalimbali za Iran kwa mnasaba wa Wiki ya Wafanyakazi na kubainisha kwamba, ukwamishaji mambo wa Wamarekani katika muamala wa kibenki ni mfano wa wazi kabisa katika uwanja wa mtazamo mbaya wa Iran kwa Marekani na kuongeza kuwa, sababu ya mabenki makubwa duniani kutokuwa tayari kushirikiana na Iran ni anga ya kuifanya Iran iogopwe iliyoletwa na inayoendelea kudumishwa na Wamarekani.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matamshi ya viongozi wa Marekani ya kudumisha vikwazo dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, viongozi hao wanadai kwamba, Iran ni nchi ambayo imekuwa ikiunga mkono ugaidi na huenda ikawekewa vikwazo kutokana na hilo na ujumbe wa maneno hayo ni kutaka nchi nyingine zisishirikiane na Iran na natija ya hilo ni kuingiwa na hofu na woga benki na wawakezaji wa kigeni wa kushirikiana na Iran.

Ayatullah Khamenei amebainisha kwamba, Wamarekani wanadai kuwa, sababu ya mataifa ya kigeni kutoshirikiana na Iran ni hali ya ndani ya taifa hili katika hali ambayo kwa sasa katika Mashariki ya Kati hakuna nchi yenye amani na usalama kama Iran. Kuhusiana na suala la ugaidi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Wamarekani ndio magaidi wabaya zaidi na kwa mujibu wa ripoti zilizopo wangali wanaunga mkono makundi ya kigaidi.

3492621

captcha