IQNA

Swala ya Kwanza ya Idul Adha katika Msikiti wa Hagia Sophia, Uturuki

13:04 - July 31, 2020
Habari ID: 3473018
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Uturuki leo wameshiriki katika Swala ya kwanza ya Idul Adha katika Msikiti wa Hagia Sophia mjini Istanbul.

Swala ya kwanza ya Ijumaa iliswaliwa katika Msikiti wa Hagia Sophia, Istanbul Uturuki baada ya zaidi ya miaka 86 ambapo maelfu ya waumini wameshiriki katika swala hiyo mnamo Julai 24, 2020.

Mapema mwezi huu,  Mahakama ya juu zaidi nchini Uturuki iliidhinisha jumba la makumbusho la Hagia Sophia kugeuzwa kuwa msikiti na kubadilisha hadhi yake ya sasa kama jumba la makumbusho.

Baraza la kitaifa la Uturuki lilikubali ombi la mashirika kadhaa yakiliomba kufuta uamuzi wa serikali wa tangu mwaka 1934 unaolipa jumba la Hagia Sophia huko Istanbul hadhi ya jumba la makumbusho.

3913732

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha