IQNA

Mkenya ashika nafasi ya tatu Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanawake Dubai

20:03 - November 28, 2021
Habari ID: 3474613
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa Duru ya Tano ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanawake Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wametangazwa.

Katika sherehe hiyo iliyofanyika Jumamosi, Neda Mohammed Fathy wa Misri ametangazwa kuwa mshindi huku nafasi ya pili ikishikwa na Rowaida Qassim Mohammad wa Marekani naye Mona Abdi wa Kenya ameshika nafasi ya tatu.

Waliofuata kwa taratibu walikuwa ni wawakilishi wa Algeria, Jordan, Afghanistan, Cameroon, Senegal, Nigeria na Mauritania.

Majaji katika mashindano hayo walikuwa ni kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Misri, Indonesia na Pakistan. Mashindano hayo yameandaliwa na Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA).

Hii ni taasisi ambayo huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanawake ya Dubai kila mwaka na mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika kutokana na janga la COVID-19.

4016485

captcha