IQNA

Wanawake kutoka nchi 50 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai

21:41 - November 16, 2021
Habari ID: 3474566
TEHRAN (IQNA)- Wawakilishi wa nchi takribani 50 wametangaza kuwa tayari kushiriki katika Duru ya Tano ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Wanawake Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)

Ibrahim Bu Milha, Mshauri wa Mtawala wa Dubai katika Masuala ya Utamaduni na Ubinadamu ambaye pia ni mwenyekiti wa   Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) amesema mashindano hayo yataanza Nogemba 20.

Ameongeza kuwa yamkini idadi ya washiriki ikaongezeka katika siku zijazo huku akibaini kuwa wageni wanaoshindana wataanza kuwasili Dubai Jumatano. Aidha amedokeza kuwa majaji katika mashindano hayo ni wasomi na wataalamu wa Qur'ani kutoka UAE, Saudi Arabia, Indonesia, na Pakistan.

Alisema washiriki wanapaswa wana umri wa miaka 25 au chini na waweze kuhifadhi Qur'ani nzima na kuzingatia sheria za Tajweed.

DIHQA ni taasisi ambayo huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanawake ya Dubai kila mwaka na mwaka jana mashindano hayo hayakufanyika kutokana na janga la COVID-19.

/3476513

captcha