IQNA

Mashindano ya Qur’ani kwa wasichana yakamilika UAE

22:46 - March 03, 2022
Habari ID: 3475000
TEHRAN (IQNA)- Duru ya 22 yla shindano la Qur'ani kwa vijana wa kike lilihitimishwa Jumatano huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Hafla hiyo iliandaliwa na Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai na washiriki walishindana katika kategoria tofauti.

Akihutubia hafla ya kufunga, naibu mkuu wa harakati ya wanawake huko Dubai, Khawla Saeed Al Naboodah alisema kuwa mashindano hayo yanasaidia kuimarisha utamaduni wa Kiislamu na kuwahimiza wengine kuhifadhi Qur'ani.  Akithamini jitihada za waandaaji, alisema pia kwamba mashandano hayo yatamridhisha Mwenyezi Mungu.

Fatima Ibrahim Muhammad Ibrahim kutoka Wakfu wa Qur'ani Tukufu na Sunnah huko Sharja, Aisha Muhammad Hussein Abdullah Al-Bahri kutoka Kituo cha Muhammad bin Salem bin Bakheet, Aisha Al Sibai Muhammad Muhammad Al-Bassiouni  kutoka moja ya Vituo vya Maktoum kwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Taif Saud Muhammad Kulaib Al Tunaiji kutoka Taasisi ya Ras Al Khaimah ya Qur'ani Tukufu na Sayansi Zake, Soraya Ahmed Ali Al Shehhi kutoka Vituo vya Maktoum kwa ajili ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu, Zainab Askar Ahmed. Massad Muhammad kutoka Kituo cha Riyadh Al-Salihin cha kuhifadhi Qur'ani Tukufu, na Hoor Jamal Ahmed Al-Ajeel Al-Tunaiji kutoka Taasisi ya Ras Al-Khaimah ya Qur'ani Tukufu na Sayansi zake walishinda tuzo za juu za makundi sita ya shindano hilo.

4040071

captcha