IQNA

Mashidano ya Qur'ani Tukufu

Mashindano ya Qur'ani Tukufu kwa wanaume, wanawake yaanza Dubai Leo

21:24 - January 07, 2023
Habari ID: 3476371
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 23 la Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum yameanza leo katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE)

Hafla hiyo ya Qur'ani kwa wanaume na wanawake itaendeshwa katika maeneo tofauti huko Dubai kwa siku tano.

Kwa mujibu wa Ibrahim Mohamed Bu Melha, mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Utamaduni na Kibinadamu na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA), jopo mbili za majaji wa wanaume na wanawake zimeundwa kutathmini washiriki wa mashindano hayo.

Amesema mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum ni miongoni mwa matukio makuu ya Qur'ani yanayoandaliwa na DIHQA kila mwaka.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yanalenga kuwahimiza raia wa UAE na wataalam kutoka nje kujifunza, kuhifadhi na kusoma Qur'ani na kufanyia kazi mafundisho yake.

Washiriki wa shindano hilo wanatakiwa kuwa na ujuzi mkubwa wa sheria za Tajweed.

Kategoria za mashindano hayo ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu, kuhifadhi Juzuu 20 (, kuhifadhi Juzuu 10, kuhifadhi Juzuu tano (kwa raia wa Imarati), kuhifadhi Juzuu tano (kwa wakaazi zaidi ya miaka 10, na  kuhifadhi Juzuu 100 kwa raia walio na umri wa zaidi ya miaka 10.

4112634

captcha