IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wawakilishi wa nchi 136 kushiriki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wasichana UAE

14:32 - August 17, 2022
Habari ID: 3475634
TEHRAN (IQNA) – Toleo la sita la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Sheikha Fatima Bint Mubarak kwa wasichana litafanyika Oktoba mwaka huu kwa kushirikisha nchi 136 katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Hayo yametangazwa na Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA), ambayo inaongoza mashindano hayo.

Ibrahim Mohammed Bu Melha, Mshauri wa Mtawala wa Dubai kwa Masuala ya Utamaduni na Kibinadamu na Mkuu wa kamati ya maandalizi ya DIHQA, alisema maandalizi ya hafla hiyo yalianza mapema na nchi 136 zitashiriki.

Idara za tuzo hiyo zitatayarisha mipango ya utendaji ya kuandaa hafla hiyo kwa njia bora zaidi, Bu Melha alisisitiza, akibainisha kuwa itaanza tarehe 28 Septemba na kuwasili kwa washiriki na wajumbewa jopo la majaji.

Mashindano hayo yataanza rasmi  Oktoba 1 na kumalizika Oktoba 5, 2022 huku sherehe ya kufunga ikipangwa kufanyika Oktoba 7, aliongeza zaidi.

Kisha Bu Melha alielezea masharti ya shindano hilo, ikiwa ni pamoja na kuwataka wagombea wawe na umri wa miaka 25 au chini ya hapo na wawe wamehifadhi Qur'ani Tukufu kwa ukamilifu kwa sauti.

Mshindi atapata AED250,000; nafasi ya pili itapata AED200,000; nafasi ya tatu AED150,000; nafasi ya nne AED65,000; nafasi ya tano AED60,000; nafasi ya sita AED55,000; nafasi ya saba AED50,000; nafasi ya nane AED45,000; nafasi ya tisa AED40,000; na nafasi ya 10 itapokea AED35,000.

3480127

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha